Jumapili , 3rd Aug , 2014

Mkutano mkuu wa klabu ya Simba uliokuwa na ajenda 13 umefanyika hii leo kwa mafanikio makubwa baada ya mambo muhimu kuafikiwa na kupitshwa na wanachama wengi waliohudhuria mkutano huo na kubwa zaidi ni wanachama hao kuazimia kuwafukuza wenzao 72

Mmoja wa wanachama wa klabu ya Simba waliofukuzwa uanachama Michael Wambura mwenye suti.

Wanachama 72 akiwemo aliyekuwa mgombea wa urais wa klabu ya soka ya Simba wamefukuzwa na kufutwa uanachama wa klabu hiyo rasmi hii leo kutuatia kuvunja katiba baada ya kuishitaki klabu hiyo mahakamani wakipinga mchakato wa uchaguzi mara baada ya wajumbe wa mkutano mkuu wa klabu hiyo kufanya maamuzi hayo hii leo jijini Dar es salaam

Mwenyekiti wa mkutano huo Rais wa klabu ya Simba Evans Aveva amesema maamuzi hayo ni kwa mujibu wa katiba ya Simba, katiba mama za Shirikisho la soka nchini TFF, Shirikisho la soka Afrika CAF hali kadhalika shirikisho la Soka Duniani FIFA ambayo yanakataa masuala ya kimichezo kupelekwa mahakamani

Aidha Aveva amesema uamuzi huo wa wanachama ni haki yao kikatiba kwakuwa ndicho chombo kinachoweza kuamua hatma ya wanachama hao ama kutoa uamuzi wa mwisho na amekili kujaribu kwa mara kadhaa kutaka suluhu na wanachama hao nje ya mahakama ili kuwasafisha lakini juhudi hizo ziligonga mwamba na hivyo uongozi wake unabariki maamuzi hayo ya wanachama wa klabu ya Simba waliyochukua katika mkutano mkuu hii leo

Na kwa upande wao wanachama Chuma Seleman [bi hindu] Hemed Rajabu pamoja na Masoud Ndete wamesema uamuzi wa wamachama wote zaidi 860 waliohudhuria mkutano huo wameupokea kwa mikono miwili maamuzi hayo na wakisema kitendo hicho kimeinusuru klabu yao kufutiwa uanachama wa TFF kama wasingefikia maamuzi hayo.