Jumatatu , 17th Nov , 2014

Vijana wanne wanatarajia kushiriki mashindano ya kuogelea ya Dunia yanayotarajiwa kufanyika Desemba 3 mpaka 7 mwaka huu nchini Katar.

Akizungumza na East Africa Radio,Katibu mkuu wa Chama cha Kuogeloea Nchini TSA,Noel Kihunsi amesema washiriki hao wameshaanza mazoezi katika vilabu vyao ambapo washiriki wengine wanafanya mazoezi katika vilabu vyao vilivyo nje ya nchi.

Kihunsi amesema washiriki hao wanatarajia kuondoka nchini kuelekea nchini Katar Desemba mosi mwaka huu na wanatarajiwa kuwasili nchini humo Desemba mbili ili kujiandaa na mashindano hayo.