Alhamisi , 16th Jun , 2016

Wakiwa na furaha kubwa umati wa watoto walijumuika kwa pamoja katika Tamasha maalumu la michezo la kumbukumbu ya vifo vya watoto wenzao waliouawa kikatili nchini Afrika Kusini mnamo mwaka 1976, siku hyo inajulikana kama Siku ya Mtoto wa Afrika.

Baadhi ya watoto wakishiriki katika michezo siku ya mtoto wa Afrika

Zaidi ya watoto 800 hii leo wameshiriki katika tamasha maalumu la maadhimisho ya kumbukumbu ya mauaji ya watoto nchini Afrika Kusini yaliyotokea miaka 40 iliyopita.

Maadhimisho ya siku hiyo hufanyika kila mwaka barani Afrika kila ifikapo Juni 16 na kila nchi hufanya maadhmisho kwa namna tofauti ilimradi kuenzi siku hiyo kwa jumbe mbalimbali zakuwahamasisha watoto juu ya haki zao na pia kuwakumbusha wazazi na wengine wote juu ya haki za watoto duniani.

Baadhi ya watoto hao wanazungumzia Tamasha hilo kubwa la michezo lililofanyika katika viwanja vya JMK Park Kidongo Chekundu jijini Dar es Salaam likiandaliwa na na Taasisi ya kulinda watoto ya Save the Children.

Wakizungumza kwa hisia na kwakujiamini baadhi ya watoto wamewakumbusha walezi kuwatimizia haki zao za kimsingi ikiwemo kuwapa elimu bora na pia kuwapa fursa ya kushiriki michezo ili kuinua na kuvumbua vipaji vyao katika michezo.

Aidha watoto hao wamekwenda mbali zaidi na kuitaja michezo kuwa ni moja ya sekta nyeti kwa sasa duniani kote na imekuwa ni moja ya sehemu kubwa ya kuongeza kipato kwa mshiriki [mchezaji] lakini kwa uchumi wa nchi.

Wamesema samani ya mtoto ni kuheshimiwa lakini kupewa haki ya kupata vitu muhimu vya kimasiha ikiwemo fursa ya kucheza michezo ambayo pengine ikawa ndiyo ajira na wakitolea mifano mingi kwa wanamichezo wanaofanikiwa na matajiri kupitia michezo ya soka, tenisi, riadha na mingine mingi ambayo wachezaji waliocheza kwa kiwango cha juu wametajirika nayo.

Wakimalizia watoto hao wamesema pamoja nakuomba watoto kulindwa na kupewa haki zao za kimsingi lakini pia wametoa wito kwa wazazi kuwapa fursa watoto kushiriki masuala mbalimbali yakiwemo ya kimichezo na ya kijaamii na pa wamegusia kugushwa na kitendo cha Serikali kusitisha michezo mashuleni jambo ambalo wamelitafsiri kama kuwakosesha haki yao ya kimsingi watoto ambao wengi wao wanapenda shule kwaajili ya kushiriki michezo.