Jumatano , 15th Apr , 2015

Mashindano ya mpira wa wavu wa ufukweni kanda ya tano kwa ajili ya kuwania nafasi ya kushiriki mashindano ya Afrika yanatarajiwa kuanza kutimua vumbi Aprili 17 mwaka huu katika fukwe za jijini Dar es salaam.

Akizungumza na East Africa Radio, makamu mwenyekiti wa Chama cha Mpira wa Wavu Nchini TAVA, Muharame Mchume amesema, mashindano hayo yatakayomalizika Aprili 19 mwaka huu yatashirikisha timu kutoka nchi zote zilizo kanda ya tano.

Mchume amesema, mpaka sasa ni nchi sita ambazo ni Uganda, Misri, Sudan, Ethiopia, Rwanda, Kenya na wenyeji Tanzania ambapo timu hizo zinatakiwa kuwasili nchini kuanzia kesho kwa ajili ya maandalizi ya mashindano hayo ya kufuzu mashindano ya Afrika yanayotarajiwa kufanyika Septemba 4-19 mwaka huu nchini Congo Brazzaville