Ijumaa , 4th Jul , 2014

Kocha wa vijana chipukizi wanaotarajiwa kushiriki michuano ya mpira wa wavu ya klabu bingwa ya mkoa wa Dar es salaam na ile ya shule za sekondari kutoka nchi za Afrika Mashariki Yusuph Mkarambati amesema kuna changamoto ya mahudhurio kwa wachezaji

Timu za Mpira wa Wavu zikipambana katika moja ya mchezo uliofanyika jijini Dar es salaam

Kocha wa vijana chipukizi wanaotarajiwa kushiriki michuano ya mpira wa wavu ya klabu bingwa ya mkoa wa Dar es salaam na ile ya shule za sekondari kutoka nchi za Afrika Mashariki Yusuph Mkarambati amesema kuna changamoto ya mahudhurio kwa wachezaji wanaotakiwa kufika kwa ajili ya kujinoa kujiwinda na michuano hiyo.

Mkarambati amesema hali hiyo imekuwa ikichangiwa na muingiliano wa ratiba za masomo kwa wachezaji hao ambao wengi wao ni wanafunzi wa shule mbalimbali.

Mkarambati amewataka wazazi kuwaruhusu watoto kuhudhuria mazoezi kutokana ili kufanya vizuri katika michuano hiyo mikubwa