Jumanne , 28th Mar , 2023

Waziri Mkuu wa Tanzania Kassim Majaliwa anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika pambano kati ya bondia Mtanzania  Hassan Mwakinyo dhidi ya bondia  Kuvesa  kutoka Nchini Congo ambapo katika pambano la utangulizi Waziri wa Nishati January Makamba atazichapa dhidi ya Mbunge Joseph Musukuma

Akizungumza kuhusu pambano hilo Promota wa Pambano hilo ni mbunge Sophia Mwakagenda amebainisha kuwa Lengo la pambano hilo ni Kuchangisha pesa za kusaidia kununua taulo za kike, Kwa Wanafunzi wanawake wa nyanda za juu Kusini. 

Pambano hilo kubwa litapigwa April 4, 2023 jijini katika uwanja wa Jamhuri Dodoma.