Jumamosi , 22nd Aug , 2015

Klabu ya Yanga imetwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Azam FC kwa penati 8 kwa 7 katika mchezo uliopigwa katika dimba la taifa Dar es salaam.

Klabu ya Yanga imetwaa Ngao ya Jamii kwa mara ya pili mfululizo baada ya kuifunga Azam FC kwa penati 8 kwa 7 katika mchezo uliopigwa katika dimba la taifa Dar es salaam.

Mchezo huo ambao huashiria kufunguliwa kwa Ligi Kuu Tanzania Bara 2015/16 ulimalizika kwa timu hizo kutofungana katika dakika 90, hali iliyolazimu kuingia katika hatua ya changamoto za penati.

Katika penati tano tano kila timu ilipata penati 4 na kukosa moja, ambapo kwa upande wa Yanga, Nadir Haroub ndiye aliyekuwa wa kwanza kupiga na kukosa, na baadaye mpigaji wa penati ya nne kwa upande wa Azam Pascal Wawa alikosa mkwaju wake.

Ilifuata penati moja moja ambapo Ame Ally Zungu alikosa penati ya tisa huku Yanga ikifunga penati zote.

Wafungaji
Yanga: Niyonzima, Kaseke, Tambwe, Coutinho, Mwashiuya, Kamusoko, Twitte, YondanI.
Azam: Tcheche, Bocco, Himid Mao, Morris, Mugiraneza, Nyoni, Kapombe.

Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Yanga kutwaa ngao ya jamii kwa kuifunga Azam kwani mwaka jana Yanga ilitwaa ngao hiyo kwa kuifunga Azam mabao 2-0.