Jumatatu , 2nd Sep , 2019

Kivumbi cha michuano ya Sprite Bball Kings 2019 kinaendelea kupamba moto kuelekea katika hatua ya 16 bora inayotarajia kufanyika wikiendi hii Jijini Dar es Salaam.

Wachezaji wa Yo! Street

Michuano hiyo inafanyika kwa msimu wa tatu mfululizo, ikiandaliwa na East Africa TV na East Africa Radio kwa kushirikiana na kinywaji cha Sprite.

Timu mbalimbali zilizofuzu hatua ya 16 bora zimeendelea kujigamba kuelezea maandalizi yao, ikiwa ni siku nne zimebakia kufika Jumamosi Septemba 7 na Jumapili ya Septemba 8, ambapo michezo hiyo itapigwa katika viwanja vya Don Bosco Oysterbay.

Akizungumza kuelekea mchezo huo, mwakilishi wa Yo! Street aliyefahamika kwa jina la Jovin amesema, "mimi naamini kwamba timu iliyojipanga vizuri itashida, Dream Chasers tunawajua wana timu nzuri lakini mchezo ni 'Quarter nne kwahiyo mwenye timu nzuri atashinda".

Naye mwakilishi wa Dream Chasers amesema kuwa timu yake ina vijana wengi wapato wanne kutoka Ligi ya Kikapu Dar RBA kwahiyo hakuna wasiwasi juu ya uwezo wao, wakiamini watashinda mchezo huo.