Jumatano , 30th Nov , 2022

Bondia Hassan Mwakinyo amesema amejiandaa vyema kupambana na Peter Bobson wa Marekani katika kuwania mkanda wa WBC Desemba 30 kwenye Uwanja wa Mao tse Tung, Zanzibar.

Amesema anataka kulitumia pambano hilo kuandika historia ya kuwa bondia wa kwanza kupigana tangu kuruhusiwa mchezo wa masumbwi visiwani Zanzibar.

Akizungumza na waandishi wa habari jijini hapa jana, Mwakinyo ambaye atapigana pambano hilo chini uratibu wa promota Shomari Kimbau alisema anatumia pambano hilo kurejesha heshima yake na ya Tanzania katika uso wa dunia.

Naye Kimbau amesema  Bobson kutoka Marekani yupo katika hadhi ambayo inalingana na ya Mwakinyo na kwamba anatarajia pambano hilo litakuwa na ushindani mkali.

ametolea ufafanuzi kuhusu pambano hilo kufanyika Zanzibar'' ameamua kuliandaa pambano hilo visiwani Zanzibar ili kuandika historia ya kurejeshwa masumbwi tangu yalipopigwa marufuku''