
Mwenyekiti Mbowe ametoa rai hiyo wakati alipohutubia mkutano wa hadhara, uliofanyika Uwanja wa Halmashauri ya Mji wa Bariadi mkoani Simiyu.
"Mataifa yanayojitambua duniani hayapimi utajiri wake kwa kuhesabu madini, hayapimi utajiri wake kwa kuhesabu misitu na mbuga za wanyama. Yanapima utajiri kwa namna ambavyo nchi imewekeza akili kwa watu wake.
Akizungumzia kuhusu Uchaguzi ujao, Kiongozi huyo amesema bado wanaendelea kuona maridhiano yatakapowapeleka na kwamba kwa sasa wanaangalia sheria za uchaguzi pamoja na Tume ya uchaguzi.