
Katika taarifa, msemaji wa jeshi Jenerali Maj Sylvain Ekenge amesema maafisa hao tayari wameondoka katika ardhi ya Congo.
Taarifa kutoka kwa msemaji wa jeshi la Rwanda Brig. Jenerali Ronald Rwivanga Rwanda ndiyo iliwaita maafisa hao
kwa upande wa DRC imewakataa wanajeshi wa Rwanda kuwa sehemu ya wanajeshi wa kanda linaloongozwa na Kenya waliotumwa mwaka jana katika jimbo la Kivu Kaskazini nchini DRC.
Mvutano kati ya Kigali na Kinshasa umezidi kuwa mbaya wiki iliyopita wakati jeshi la Rwanda lilipopiga kombora ndege ya kivita ya Congo karibu na uwanja wa ndege wa Goma. Utaratibu wa uthibitishaji wa kikanda umewekwa ili kuchunguza tukio hilo.