Jumanne , 30th Apr , 2024

Watu 9 wamenusurika kifo baada ya magari aina ya coaster na land cruiser kugongana katika eneo la barabara ya Kashura Manispaa ya Bukoba mkoani Kagera baada ya gari aina ya coaster kufeli breki na kuparamia nyumba.

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Akizungumzia ajali hiyo Mkuu wa wilaya ya Bukoba Erasto Sima, amesema kuwa kwenye coaster kulikuwemo watu watano na Land cruise watu wawili na kwenye nyumba walikuwepo watu wawili ila hakuna kifo na majeruhi wamekimbizwa hospital ya Rufaa ya mkoa Bukoba.