Ijumaa , 12th Apr , 2024

Mwanamke mmoja anayefahamika kwa jina Agnes Samsoni mkazi wa mtaa wa Nyantorotoro Halmashauri ya mji Geita anaiomba Serikali na wasamaria kumsaidia kupata fedha za vipimo na matibabu ya mtoto wake Brytone Silvester (9) ambaye hatembei wala kuongea baada ya kuugua kwa muda mrefu.

Bi. Agnes Samsoni mkazi wa Nyantorotoro, Geita ambaye amekimbiwa na mzazi mwenzake baada ya mtoto wao kuugua kwa muda mrefu.

Katika mazungumza na EATV mama amesema mtoto wake ameanza kuugua tangu mwaka 2020 licha ya jitihada zinazofanywa na familia pamoja na majirani ili kuokoa maisha ya mtoto wao familia hiyo aina uwezo wa kifedha kumpeleka mtoto huyo kwenye matibabu.

"Brytone nimemzaa akiwa vizuri tu tumekaa naye ndani ya miaka mitatu alipofikisha miaka minne akaanza kuugua ilikuwa 2020 baada ya hapo tulimpeleka hospitalini Nyankumbu akagundulika kuwa na Malaria iliyopanda kichwani ambayo inamfanya awe na degedege, alichomwa sindano baada ya hapo tukaona bado hali ni mbaya watu wakaanza kutushauri tutumie dawa za kienyeji lakini hazikusaidia" Agnes Samsoni, mama wa mtoto.

Bi. Agnes  anasema baada ya baba yake mzazi kuona changamoto ya mtoto wao kuugua bila kupona akaamua kumkimbia na amekaa kwa muda mrefu sasa hajaona hata dalili ya kurejea na amepata mwanaume mwingine ambaye anaishi naye akimsaidia matumizi ya nyumbani lakini hela ya matibabu wamekosa kulingana na kipato chao.