Alhamisi , 13th Jan , 2022

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan, amesema kuwa Urais ni taasisi na sio mtu, na kuwataka wasiompenda Rais basi waheshimu mambo yanayoizunguka taasisi hiyo pamoja na Mungu ambaye ndiye hupanga nani akae wapi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Samia Suluhu Hassan

Kauli hiyo ameitoa hii leo Januari 13, 2021, wakati akifanya mazungumzo na Mawaziri pamoja na Manaibu Waziri aliowaapisha hivi karibuni.

"Rais ni taasisi na sio mtu, ni taasisi ambayo inakuja na mamlaka yake, yoyote anayekuwepo pale anafanyia kazi taasisi ya Urais, sasa kama humpendi aliyepo penda nchi yako, tunaambiwa kwamba mamlaka na uongozi unatoka kwa Mungu," amesema Rais Samia 

Aidha ameongeza "Kama humpendi (Rais) aliyepo, mheshimu Mungu wako, kwa kujua kwamba aliyepo amewekwa na Mungu, Samia aliyepo simpendi tu, kwahiyo sio usimpende yeye ukapuuza na yote yanayozunguka taasisi aliyopo, yale yanayotokana na taasisi yaheshimu, mchukie yeye tu,".