Ijumaa , 4th Mar , 2016

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu, Sera, Bunge, Kazi, Vijana, Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenister Joakim Mhagama ametengua uteuzi wa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii (NSSF) Dkt. Carina Wangwe uliotangazwa jana Dar es salaam.

Waziri wa nchi Ofisi ya Waziri Mkuu,Sera,Bunge,Kazi,Vijana,Ajira na Wenye Ulemavu Mhe.Jenister Joakim Mhagama.

Taarifa kwa vyombo vya habari iliyotolewa usiku wa kuamkia leo , imeeleza kuwa uteuzi huo umetenguliwa kutokana na kutokamilika kwa baadhi ya taratibu ambapo uteuze huo umeweza kudumu chini ya masaa 24 tangu kuteuliwa kwake.

Kulingana na Taarifa hiyo, uteuzi mpya kwa mujibu wa mamlaka na sheria utakapofanyika taarifa zitatolewa kwa wananchi

Mapema Jana waziri Muhagama alimteua Dkt. Carina Wangwe kuwa Kaimu Mkurugenzi Mkuu wa Shirika la Hifadhi ya Jamii(NSSF) kuchukua nfasi ya Mkurugenzi wa zamani Bw. Ramadhan Dau ambae aliteuliwa hivi karibu kuwa balozi.