Alhamisi , 30th Nov , 2023

Bilionea namba 5 duniani kwa mujibu wa jarida la Forbes, Warren Buffett baada ya mwanahisa mwenzake ndani ya kampuni ya ''Berkshire Hathaway'' Bwana Charlie Munger kutangulia mbele ya haki 28/11/2023

 

Kwenye jarida la Fortune Magazine, linaeleza kuwa kwenye barua iliyochapishwa na kampuni ya ''Berkshire Hathaway'' liliandika kuhusu uamuzi ambao uliazimiwa na familia hiyo tangu mwaka 2006 kuhusiana na kugawa mali za bilionea huyo kwa masikini.

Uamuzi ambao ulijadiliwa tena November mwaka huu pamoja na watoto wake watatu ambao wanakadiriwa kuwa na umri kati ya miaka 65 - 70, ni kuhusu kugawa asilimia 99 ya utajiri wa Bilionea huyo kwa familia masikini na watoto wake kuhakikisha hilo linafanyika kwa usimamizi wao.

Unahisi kwa hapa kwetu Tanzania lingekubalika hili?, mzazi kugawa mali zake kwa familia masikini ili hali watoto wake wapo hai?

Siyo vibaya ukatuandikia mtazamo wako, kwenye hili.
 
Chanzo: Fortune Magazine.