Jumatatu , 14th Jul , 2014

Chama cha mchezo wa cricket Tanzania TCA kimetangaza wachezaji 14 wapya watakaounda kikosi cha timu ya taifa ya cricket ya vijana kitakachokwenda kwenye mashindano ya vijana ya Afrika yatakayofanyika nchini Zambia

Wachezaji wa cricket wakiwa katika moja ya michezo hapa nchini.

Wachezaji 14 wa mchezo wa cricket wameteuliwa kuunda kikosi cha timu ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 18 kikosi ambacho kitashiriki michuano ya kusaka tiketi ya kucheza mashindano ya dunia,

Kocha wa kikosi hicho Kharil Rhemtula amesema awali walichagua wachezaji wa umri chini ya miaka 19 lakini kutokana na mashindano ya dunia kufanyika mwakani wameona wachague wachezaji wa umri chini ya miaka 18 ambao ikifika mwakani watakuWa na umri unaotakiwa kushiriki michuano ya dunia ya umri chini ya miaka 19

Aidha Rhemtula amesema tayari kikosi cha wachezaji hao kimeanza mazoezi rasmi kujiandaa na mashindano ya kufuzu yatakayofanyika jijini Lusaka Zambia kuanzia August 7 mwaka huu.