Jumapili , 8th Jun , 2014

TSA yasema kozi ya ukocha wa mchezo wa kuogelea level three ni ya kiwango cha juu katika mchezo huo yawataka walimu wa mchezo wa kuogelea kuchangamkia fulsa hiyo

Waogeleaji wa Tanzania wakichuana katika moja ya mashindano yakuogelea yaliyoandaliwa na TSA.

Chama cha kuogelea nchini Tanzania TSA kinataraji kuendesha kozi ya makocha wa mchezo wa kuogelea level three kozi ambayo itaanza june 20 mwaka huu ikishirikisha makocha wa mchezo wa kuogelea toka Tanzania bara na visiwani

Katibu mkuu wa TSA Noel Kihunsi amesema kozi hiyo itakayochukua siku 10 itaongozwa na mkufunzi wa shirikisho la kimataifa la kuogelea FINA toka nchini Ujerumani Martius na tayari wao TSA kama chama wameshatuma mialiko kwa walimu wote wa mchezo wa kuogelea Tanzania bara na visiwani na mwisho wa kuthibitisha ushiriki ni june 15 mwaka huu ikiwa ni siku tano kabla ya kuanza kwa kozi hiyo

Aidha Kihunsi ametoa wito kwa walimu wote ambao wanataka kushiriki kozi hii ya level three ambayo ni kozi ya juu katika mchezo wa kuogelea basi wafanye hivyo kabla ya zoezi hilo halijafungwa rasmi june 15 mwaka huu.