Jumatatu , 27th Apr , 2015

Kozi ya waamuzi wa mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam inatarajia kuanza hapo kesho kwa kushirikisha waamuzi takribani 30.

Akizungumza na East Africa Radio, Mwenyekiti wa kamati ya ufundi wa chama cha mpira wa wavu mkoa wa Dar es salaam DAREVA, Nassoro Shariff amesema, kozi hiyo yenye lengo la kupata waamuzi wengi ambao sio wachezaji itamalizika Mei mbili mwaka huu.

Shariff amesema, kozi hiyo itachukua waamuzi wengi ambao sio wachezaji kwani waamuzi ambao ni wachezaji wengi wao wanachezesha wakiwa wametoka kucheza hivyo wanashindwa kuchukua maamuzi katika mechi anayochezesha.