Ijumaa , 24th Sep , 2021

Kocha mkuu wa Yanga SC, Mohamed Nabi amesema kuwa wamejiandaa vyema kuelekea mchezo wa Jumamosi ya kesho Septemba 25, 2021 wa Ngao ya Jamii dhidi ya Simba SC huku akiweka wazi kuwa atatoa nafasi kwa wachezaji wanaostahili kuanza mchezo huo.

Kocha wa klabu Yanga, Mohammed Nasreddine Nabi akiongea mbele ya Wanahabari.

Nabi amesema kauli hiyo leo Septemba 24, 2021 mbele ya waandishi wa Habari kuwa kikosi kipo na hali nzuri kuelekea mchezo mkubwa unaofuatiliwa ndani na nje ya Tanzania, huku akionesha hali kusikitishwa na kanuni ya kutumia wachezaji nane tu kwenye michezo iliyopo chini ya TFF, huku akisema hana budi kuheshimu sheria iyo.

Mtunisia huyo amewaomba wanayanga wawe na uvumilivu kuelekea msimu mpya kwakuwa wanakikosi kizuri kuelekea msimu mpya na pindi pale timu itakapokuwa namuunganiko mzuri itakuwa tishio sana.

Pia amewashukuru viongozi wa Yanga kwa kufanya usajili wa viwango vikubwa pamoja na kuwa wavumilivu pindi matokeo yaponakuwa sio ya kuridhisha hii ikiwemo pamoja na kutolewa kwenye mashindano ya ligi ya mabingwa kwenye hatua za awali msimu huu. 

Kwenye hali za majeruhi, Nabi ametabanaisha kuwa wachezaji kama Balama Mapinduzi aliyekosa msimu uliopita na Yassin Mustafa aliyekaa nje kwa miezi sita kabla ya msimu kutamatika, watahitaji kupitia maandalizi na mazoezi mepesi kabla ya kurejesha katika hali ya ushindani.

Vile vile Yanga, watamkosa Mukoko Tonombe, ambaye alipewa kadi nyekundu katika fainali hiyo baada ya kupiga kiwiko kwa makusudi nahodha wa Simba, John Bocco na kupelekea mwamuzi wa mchezo huo Ahmed Arajiga kumtoa nje.

Kuelekea michezo huu wa kukata na shoka pande zote mbili zimefanya usajili yakinifu kuelekea msimu mpya, hivyo nafasi za wachezaji hawa wawili kwa timu zote mbili hazitakuwa na kazi ya kuziziba pindi watakapo shuka kugombea taji la kwanza la msimu huu.