Jumanne , 14th Apr , 2015

Shirikisho la Soka nchini TFF limesema kozi ya waamuzi vijana itasaidia waamuzi kuweza kutafsiri na kuzitumia sheria pale wanapokuwa katika kiwanja cha mpira na kuweza kupunguza makosa watakapokuwa na umri kubwa.

Akizungumza na East Africa Radio, mkufunzi wa mafunzo ya waamuzi kwa vijana chini ya miaka 17, Sudi Abdi amesema, mafunzo ya uamuzi katika umri mdogo yanasaidia kwani anaweza kuelewa na kutumia sheria kwa urahisi bila kuzipindisha.

Abdi amesema, kozi hiyo ya vijana iliyoshirikisha vijana 27 ambapo itafanyika kwa muda wa siku tano kuanzia hapo jana itawasaidia kukaa na umri mrefu katika kiwango hicho na kuweza kufikia ngazi za uamuzi wa Shirikisho la Soka Ulimwenguni FIFA akiwa na umri mdogo.