Jumatano , 27th Mei , 2015

Timu ya taifa ya ngumi inaondoka leo kuelekea nchini Zambia kwa ajili ya kushiriki michezo ya kujipima nguvu itakayowasaidia katika michuano ya kimataifa iliyopo mbele yao.

Katika taarifa yake, Katibu Mkuu wa Shirikisho la Ngumi za Ridhaa nchini BFT, Makore Mashaga amesema, kikosi cha timu ya Taifa kinakwenda Zambia baada ya kupata mualiko kutoka nchini humo.

Mashaga amesema, timu inakabiliwa na michuano ya kimataifa ya Afrika AAG inayotarajiwa kufanyika Septemba mwaka huu Congo Brazzaville hivyo mashindano hayo ya kujipima nguvu yatasaidia kuwaweka fiti mabondia hao.