Ijumaa , 2nd Dec , 2022

Mchezaji Simba SC, Gadiel Michael amefungiwa michezo mitatu (3) na kutozwa faini ya Sh. 500,000 (laki tano) na TPLB kwa kosa la kulazimisha kuingia uwanjani saa 4:25 asubuhi ya siku ya mchezo wa sare ya 1-1 dhidi ya Mbeya City kwa kile alichoeleza alitaka kukagua kiwanja.

Licha ya walinzi wa uwanja huo kumzuia Gadiel (ambaye alikuwa ameongozana na watu kadhaa waliovalia fulana zenye nembo ya klabu ya Simba), kwasababu haukuwa muda rasmi kwa ajili ya zoezi hilo na Simba hawakufanya mawasiliano yoyote na Kamishna wala Mratibu wa Mchezo wakieleza jambo hilo, Gadiel alitumia hila na kufanikiwa kuwakwepa walinzi hao kisha kuingia kiwanjani.

Mchezaji huyo alipoingia kiwanjani hakuonesha dalili yoyote ya kukagua eneo la kuchezea na badala yake alionekana kwenda moja kwa moja hadi eneo la katikati ya kiwanja na kumwaga vitu vyenye asili ya unga.