Jumamosi , 25th Jun , 2016

Timu ya Taifa ya Uganda katika CECAFA sasa wametupwa kundi la kifo na timu za Ghana na Misri ambazo zimekuwa zikizisumbua sana katika michuano ya CECAFA.

Timu ya taifa ya Uganda, maarufu The Cranes.

Timu ya taifa ya Uganda, maarufu The Cranes imepangwa katika Kundi E pamoja na Ghana, Misri na Kongo katika hatua ya mwisho ya mchujo wa kuwania tiketi ya Kombe la Dunia mwaka 2018 nchini Urusi.

Uganda ndiyo nchi pekee ya Afrika Mashariki na Kati, ukanda ulio chini ya CECAFA iliyobaki katika mbio za Kombe la Dunia 2018 nchini Urusi.

Kundi A lina timu za Tunisia, Libya, Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo na Guinea, Kundi B kuna Zambia, Cameroon, Algeria na Nigeria, Kundi C kuna Gabon, Mali, Ivory Coast na Morocco, wakati Kundi linaundwa na Senegal, Afrika Kusini, Burkina Faso na Cape Verde.

Mechi za kwanza za makundi zitachezwa Oktoba mwaka 2016 na mshindi wa kila kundi ndiye atakayefuzu kuiwakilisha Afrika kwenye fainali hizo.

Lakini wadau wa soka wanaitazama Uganda kama timu ambayo pamoja na kuchululiwa kama wasindikizaji ama wasiopewa nafasi kubwa [underdogs] katika kundi hilo lakini katika mpira hakuna timu ndogo hivyo lolote linaweza kutokea katika soka mchezo ambao mara nyingi umekuwa na matokeo yasiyotarajiwa na unamiujiza yake.