Jumanne , 29th Mar , 2016

Baada ya kutokuwepo kwa ushirikiano wa kutosha katika masuala la kiufundi baina ya vyama vya michezo mbalimbali nchini na mashirikisho ya michezo kwa shule za msingi na Sekondari[ UMISETA NA UMISHUMTA] BMT yataka ushirikiano uanzishwe tena baina yao.

Baadhi ya wanafunzi wa timu za UMISETA wakiimba wimbo wa taifa katika moja ya mashindano hayo.

Baraza la michezo nchini Tanzania BMT limesema ni wakati sasa kwa vyama vya michezo kujihusisha katika mashindano ya yanayouhisha mashirikisho ya michezo ya shule za Sekondari UMISETA na shule za msingi UMITASHUMTA ili kusaka vipaji na kuviendeleza.

Akizungumza hii leo ofisini kwake jijini Dar es Salaam katibu mkuu wa baraza la michezo nchini BMT Mohamed Kiganja amesema zamani ilikuwa rahisi kwa wanamichezo kugundulika kirahisi ama kuvumbuliwa vipaji vyao kwakuwa wakufunzi ama wataalamu kutoka vyama vya michezo mbalimbali walikuwa wakishiriki na kutoa ushirikiano wa masuala ya kiufundi na pia kushiriki katika suala la ung'amuzi wa vipaji vipya.

Aidha Kiganja amesema ni vyema vyama vya michezo vikatoa ushirikiano wa kiufundi katika mashindano hayo ya wanafunzi badala ya kukaa pembeni kwasababu eti hawasimamii moja kwa moja michuano hiyo huku akitolea mfano ilivyokuwa zamani wakati wakiwaalika TFF kushirikiana nao kiufundi katika michuano hiyo.

Kiganja amesema mashindano hayo yamekuwa na mafanikio sana kwa siku za nyumba na kuibua vipaji vya wanasoka wengi na wanamichezo wa michezo mingine mbalimbali waliovuma na wanaovuma kwa sasa katika medani za kitaifa na kimataifa akimtolea mfano Kipa chipukizi wa timu ya Simba Manyika Peter Manyika jr.

Akimalizia Kiganja amesema wakati huu kamati mbalimbali za michezo kutoka wizara zinazohusika na mashindano ya mashule [UMISETA na UMITASHUMTA] kama TAMISEMI wanajipanga ni vyema vyama vya michezo vikaandaa wataalamu wa kiufundi kwaajili yakushirikiana na mashirikisho hayo ya michezo kwa shule za Msingi na Sekondari.