Ijumaa , 17th Jun , 2016

Ni wazi kuwa hakuna Mtanzania asiyeguswa na matokeo mazuri ya vijana wa timu ya soka ya taifa ya vijana chini ya umri wa miaka 17 Serengeti Boys wanayopata kwa sasa tangu kuteuliwa kuunda timu hiyo kwaajili ya michuano ya kimataifa msimu huu

Kocha wa Serengeti Boys Bakari Shime [kulia] na viongozi wengine wa tiimu hiyo na TFF.

Kocha wa Serengeti Boys ambayo inajianda na mchezo wa kufuzu kwa AFCON dhidi ya Shelisheli ametoa wito kwa Watanzania kuisaidia timu hiyo ambayo imeonyesha mwelekeo wakufanya vizuri.

Bakari Shime ametoa wito kwa Watanzania kuiangalia kwa jicho la huruma na kuisaidia timu hiyo ili ifanye vema katika michuano ya kimataifa badala ya kuliachia peke yake shirikisho soka nchini Tanzania TFF ambalo kwa sasa liko katika hali mbaya kifedha.

Shime amesema kiukweli Watanzania bila kujali tofauti zao za aina yoyote wanapaswa kuunga mkono juhudi za vijana hao ambao tangu kuitwa kwao wameonyesha mwanga baada ya kufanya vizuri katika michezo yote waliyocheza kuanzia ya ndani na ile ya nje ikiwemo ya ushindani na ya kiarafiki.

Timu hiyo ambayo ilikwenda kushiriki michuano ya kiamtaifa ya mwaliko ya mataifa matano kutoka mabara ya Ulaya, America, Asia na Afrika iliyofanyika nchini India na kuambulia nafasi ya tatu ikiwa haijapoteza mchezo hata mmoja ikishinda na kuambulia sare, tayari imeingia kambini mwanzoni mwa juma hili jijini Dar es Salaam tayari kujiwinda na mchezo muhimu wakufuzu kwa michuano ya mataifa ya Afrika kwa vijana AFCON U17 dhidi ya Shelisheli mchezo utakaopigwa Juni 25 mwaka huu jijini Dar es Salaam na baade kurudiana Julai 2 mwaka huu huko Shelisheli.

Akimalizia Shime ambaye aliwahi kuwa kocha mkuu wa timu ya maafande wa JKT Mgambo ya Tanga amesisitiza sapoti ya kutosha kwa vijana hao ambao baadae watakuwa hazina kubwa kwa taifa na hasa ikizingatiwa timu hiyo haina udhamini wowote kitu ambacho kinapelekea hata wao walimu kushindwa kutimiza sawasawa mipango[ programu] yao ya maandalizi kwakutegemea shirikisho pekee ambalo kwa sasa haliko vizuri kifedha na hata kufikia baadhi ya mali za shirikisho hilo [TFF] kutaifishwa na mamlaka ya mapato [TRA].