Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Biashara ya Kaboni kuingiza Pato la Taifa

Jumatatu , 5th Feb , 2024

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo amesema Serikali inatarajia kupata wastani wa shilingi trilioni 2.4 kutokana na biashara ya kaboni ambazo zitachangia kwa kiasi kikubwa kwenye pato la Taifa.

Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira) Mhe. Dkt.Selemani Jafo

Dkt. Jafo ameliarifu Bunge leo Februari 5, 2024 wakati akijibu swali la Mbunge wa Buhigwe Mhe. Kavejuru Felix aliyetaka kujua biashara ya kaboni katika misitu ya asili na ya kupanda imechangia kiasi gani kwenye pato la taifa tangu iingie nchini.

Wamesema hadi kufikia Desemba 31, 2023 Serikali imepokea jumla ya maombi 35 ya miradi mbalimbali ya biashara hiyo pindi mchakato wa usajili utakapokamilika na kuanza kutekelezwa kwa miradi hii.

"Katika miaka ya hivi karibuni kumeibuka soko huria la biashara ya kaboni ikijumuisha misitu ya asili na ya kupanda na imeanza kushamiri hapa nchini na kuonesha inaweza kuchangia kwenye Pato la Taifa," amesema Dkt. Jafo.

Halikadhalika, Waziri Jafo alisema katika kipindi cha mwaka 2018-22 fedha zilizopokelewa kupitia miradi inayotekelezwa kwenye halmashauri mbalimbali hapa nchini inafikia shilingi bilioni 32.

Akiendelea kujibu maswali ya nyongeza kuhusu mkakati wa utoaji elimu ya biashara hiyo, Dkt. Jafo alisema kuwa Serikali kupitia Ofisi ya Makamu wa Rais kwa kushirikiana na Ofisi ya Rais – TAMISEM pamoja na Wizara ya Maliasili na Utali imefanya mkutano na wakuu wa mikoa na wilaya kupeleka ujumbe.

Aliongeza kuwa Ofisi ya Makamu wa Rais imeendelea kutoa elimu kwa wananchi na kuwahamasisha kupanda miti kwa wingi ili kunufaika na biashara hiyo na kuhifadhi mazingira.

Pamoja na hayo, Waziri Jafo alisema pia Tanzania imetumia fursa ya ushiriki katika Mkutano wa 28 Mabadiliko ya Tabianchi uliofanyika Dubai, Falme za Kiarabu kutangaza biashara ya kaboni.

Kutokana na hatua hiyo alisema kuwa mwitikio wa wananchi na kampuni za ndani na nje kushiriki katika biashara ya kaboni umekuwa mkubwa hivyo kuongeza pato la Taifa.

Hivyo, Waziri Jafo alitumia nafasi hiyo kuwasihi wabunge katika maeneo yao yaliyobarikiwa kuwa na misitu kuona kuwa ni muhimu kushiriki katika biashara hiyo ili si kuongeza pato la Taifa.

HABARI ZAIDI

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine

Kaimu Mkurugenzi wa ufuatiliaji na uzingatiaji sheria NEMC,

Wamiliki wa Hospitali nchini wapewa siku 90