Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Wauzaji mafuta holela wapewa onyo

Jumatatu , 6th Nov , 2023

Mamlaka ya Udhibiti wa Huduma za Nishati na Maji (EWURA), inatarajia kuanza udhibiti wa Biashara holela ya mafuta, ili kulinda ubora wa mafuta, usalama wa Wananchi na majanga ya milipuko yanayoweza kutokea wakati biashara hizo zikifanyika.

Hayo yamesema na Meneja wa EWURA Kanda ya Ziwa, George Mhina wakati wa uelimishaji Wananchi na Wafanyabiashara Wilaya ya Mbogwe Mkoani Geita na kuhudhuriwa na Wenyeviti wa Serikali za vijiji, Kata na Halmashauri,ambapo amesema Wilaya ya Mbogwe inaongoza kwa ufanyaji wa Biashara holela ya mafuta ikiwemo ile iliyo maarufu kwa jina la kupiga nyoka kitu ambacho ni kosa kisheria na hatari kwa usalama wa Wananchi.

Kwa upande mwingine, Mhina amewaomba wananchi kuchangamkia fursa ya kuuza mafuta kwa kuomba leseni kwani kwa  kanda ya ziwa EWURA imetoa leseni 575 na kati ya leseni hizo 26 wamiliki wamepewa barua za kujieleza ndani ya siku saba baada ya kubainika hawatoi huduma.