Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

1,000 wafanyiwa upasuaji bure kanda ya ziwa

Jumatatu , 10th Jun , 2019

Zaidi ya wakazi 1000 wa Kanda ya Ziwa wamenufaika na matibabu bure hasa kwa upande wa upasuaji unaofanywa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania

Wagonjwa wakiwa hospitali ya Bugando.

Hayo yamebainishwa na Rais wa Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania, Dkt. Catherine Mung’ong’o wakati wa siku ya kuhitimisha zoezi la upasuaji lililofanyika kwa siku tano kuanzia tarehe 03 hadi 07 Juni 2019 katika Hospitali ya Rufaa ya Bugando jijini Mwanza.

Alisema kuwa lengo la upasuaji huo ni kupunguza idadi ya wahitaji wa huduma ya upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu toka Kanda ya Ziwa, nakuongeza kuwa zoezi hilo limefanyika kwa ushirikiano baina ya Chama hicho,  Madaktari wa Hospitali ya Rufaa ya Bungando na Madaktari wengine.

Dkt. Mung’ong’o  amesema kuwa huduma hii ya upasuaji inayotolewa na Chama cha Madaktari wa Upasuaji Tanzania imekuwa ikifanyika kila mwaka katika mikoa mingine huku ni ikiwa ni mara ya kwanza katika mikoa ya Kanda ya Ziwa. 
 
Kwa upande wake Kiongozi wa Chama hicho Kanda ya Ziwa ambaye ni Daktari Bingwa wa Upasuaji toka Hospitali ya Rufaa Bugando, Dkt. Olivia Kimario amesema kuwa zoezi hilo ni utaratibu uliowekwa na Chama cha Madaktari hao ambapo mwaka huu wamehudumia katika mikoa ya Mwanza , Shinyanga , Mara na Geita.

Katika hatua nyingine Dkt. Mung’ong’o amesema kuwa baada ya kukamilisha zoezi hilo la upasuaji kwa wagonjwa wanaosubiri kwa muda mrefu Chama hicho kitatoa huduma bure za upasuaji kwa wagonjwa wenye matatizo ya Mdomo Sungura litakalofanyika tarehe 10 na 11 Juni 2019 bila ya malipo.
 

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine