Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Achaneni na mbwa aliyepotea" - Lugola

Jumamosi , 21st Jul , 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola ameitaka jamii ya kitanzania hususani waandishi wa habari kuacha kufuatilia tukio la kupotea mbwa wa Jeshi la Polisi anayejulikana kwa jina la Hobby, kwa kuwa jambo hilo kwa sasa lipo chini ya uchunguzi.

Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola akiwa pamoja na mbwa

Waziri Lugola ametoa kauli hiyo leo Julai 21, 2018 wakati alipokuwa anazungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam mara baada ya kumaliza ziara yake katika vyombo vya Ulinzi ambavyo vipo chini ya Wizara  yake na kubaini changamoto na madudu mbalimbali yaliyokuwa yakifanywa na askari hao kwenye maeneo yao ya kazi.

"Nimekubaliana na Ispekta Jenerali wa Polisi, Simon Sirro jana Julai 20, 2018 kwamba waingie kwa undani sana kufanya uchunguzi wa nini kimetokea kwenye kikosi hicho halafu baadae wanipe taarifa. Kwa hiyo jambo hili sasa linaenda kufanyiwa kazi na Inspekta Jenerali wa Polisi", amesema Waziri Lugola.

Pamoja na hayo, Waziri Lugola ameendelea kwa kusema "na nyinyi wanahabari kwa kuwa jambo hili linaenda kufanyiwa uchunguzi naomba sasa tuache kufuatilia jambo hili ili chombo husika kiweze kuchunguza halafu tuone nini cha kufanya".

Julai 19, 2018, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola alibaini upotevu wa mbwa huyo wakati alipokuwa kwenye ziara yake katika Kikosi cha Farasi na Mbwa kilichopo eneo la Bandari Jijini Dar es Salaam na kumuagiza IGP Sirro kutoa maelezo ya upotevu wa mbwa.

Mbali na hilo, Waziri wa Mambo ya Ndani, Kangi Lugola amewaonya wananchi kuacha tabia ya kupotosha taarifa na matamko yake ambayo anayatoa kwenda sehemu husika.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto