Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Afisa Mtendaji wa Kijiji ashushiwa kipigo, Vunjo

Alhamisi , 8th Jan , 2015

Wananchi wa kijiji cha Nduoni kata ya Kirua Vunjo Magharibi mkoani Kilimanjaro wamefunga ofisi ya kijiji na kumpiga afisa mtendaji wa kata hiyo kwa madai ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita.

Wananchi wa kijiji cha Nduoni kata ya Kirua Vunjo magharibi mkoani Kilimanjaro wamefunga ofisi ya kijiji na kumpiga afisa mtendaji wa kata hiyo kwa madai ya kuchakachua matokeo ya uchaguzi uliopita kwa kumtangaza mgombea wa Chama Cha Mapinduzi kuwa mshindi badala ya mgombea wa chama cha NCCR Mageuzi.

Wananchi hao walikusanyika katika ofisi ya kijiji hicho wakiwa na mabango mbalimbali na kusema kuwa wanasikitishwa na hatua ya serikali kumwapisha mgombea wa Chama Cha Mapinduzi Bw. Joseph Msaki aliyepata kura 158 na kumwacha mgombea wa chama cha NCCR mageuzi Bw. Thomas Ngowi aliyechaguliwa na wananchi kwa kupata kura 163.

Wamesema wamefikia hatua ya kufunga ofisi hiyo kwa madai ya kupewa kiongozi ambaye siyo chaguo la wananchi kwa kuwa serikali ilimwapisha kwa nguvu mgombea wa chama cha mapinduzi kuwa mwenyekiti wa kijiji hicho.

Kufuatia vurugu za wananchi hao afisa mtendaji wa kata ya Kirua Vunjo Magharibi Reginald Mlay alilazimika kumtangaza rasmi Bw. Thomas kupitia tiketi ya Chama cha NCCR Mageuzi kuwa ndiye mshindi halali wa kijiji hicho baada ya kupata kura 163 akifuatiwa na mgombea wa Chama Cha Mapinduzi aliyepata kura 158 na TLP kura Tisa

Naye mjumbe wa halmashauri kuu ya chama cha NCCR Mageuzi taifa Bw. Hemed Msabaha amesema mtendaji huyo alikiuka kanuni za uchaguzi kwa kuhujumu maamuzi ya wapiga kura jambo ambalo limesababisha vurugu ambazo zinatishia usalama.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, January Makamba,

China yaahidi kuendelea kufadhili miradi Tanzania

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali