Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Bulembo agoma kugombea CCM

Jumanne , 19th Sep , 2017

Mwenyekiti wa Jumuiya ya Wazazi wa Chama cha Mapinduzi (CCM), Alhaji Abdallah Bulembo amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo kwa madai kuwa anaamini kati ya wagombea 48 waliojitokeza wanatosha. 

Mwenyekiti huyo wa jumuiya ya wazazi CCM amesema hatogombea tena nafasi hiyo na amewasilisha barua kwa Katibu Mkuu wa CCM kutogombea nafasi ya uenyekiti wa jumuiya hiyo na kueleza kuwa awali alichukua fomu kutokana na shinikizo kutoka kwa makatibu wakuu na wazee wa jumuiya hiyo.

"Leo nimewaita kuwaeleza sitagombea tena licha ya kuchukua fomu, naamini wagombea 48 waliopatikana, kuna mmoja atatufaa kuongoza jumuiya hii, leo ninapeleka barua kwa Katibu Mkuu wa chama ya kumweleza dhamira yangu hii,” amesema Bulembo 

Bulembo amesema uchaguzi katika ngazi ya Taifa utafanyika kuanzia Novemba 20 hadi 23, wagombea wote wapo lakini yeyote aliyeanza kampeni mapema huyo atakuwa ameshajiondoa mwenyewe.  

Kuhusu hoja ya kuchukua fomu amesema haikuwa dhambi kwa kuwa kanuni za chama zinaruhusu na upo uwezekano wa kuwa na nafasi mbili za uongozi.

"Kumekuwa na upotoshaji kwamba, ukiwa mbunge au waziri hauwezi kugombea nafasi nyingine,  hapa nina kitabu cha kanuni za mwaka 2005, 2010, 2012 na 2017 zinasema kiongozi au mbunge, waziri anaweza kugombea lakini kamati kuu ya chama itaamua inavyofaa, kama bado anahitajika atapitishwa lakini kwa upande wangu sitagombea" amesema.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto