Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

CHADEMA yawavua nyadhifa Kubenea na Komu

Alhamisi , 18th Oct , 2018

Baada ya kikao cha Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA),kuwahoji wabunge wake wa Moshi Vijijini Antony Komu na Saed Kubenea wa Ubungo kuhusu kuvuja kwa sauti wakipanga njama za kumuondoa Meya wa Ubungo Jacob Boniphace,

Wabunge wa CHADEMA, Anthony Komu (kushoto) na Saed Kubenea (kulia)

 CHADEMA wameazimia kuwavua nyadhifa zote za uongozi ndani ya chama

Akizungumza na wanahabari, Naibu Katibu Mkuu Bara John Mnyika amesema kuwa, Kamati Kuu ya chama iliwaita wabunge hawa kuja kujieleza juu ya tuhuma ya utovu huo wa nidhamu, na walifika kujieleza, na walikiri kwamba ni sauti zao.

Mnyika amesema Kamati kuu imewakuta na hatia, imefanya maamuzi ya adhabu juu yao, "mosi imefikia uamuzi wa kuwapa onyo, pili imewataka waandike barua ya kuomba radhi kwa chama., tatu Kamati kuu ikafikia uamuzi wa kuwaweka kwenye uangalizi kwa miezi 12, na nne ikafikia uamuzi wa kuwavua nafasi zao zote za uongozi ndani ya chama na kubaki na ubunge"

Pia wabunge hao Antony Komu na Saed Kubenea ambao pia wamehudhuia mkutano huo, wametakiwa kujitokeza mbele ya umma na kuomba radhi.

Kubenea na Komu sauti zao zilianza kuzagaa Jumapili ya Oktoba 14, kwenye mitandao ya kijamii ambapo moja kati ya mazungumzo yao walidai kuwa Meya Boniphace Jacob wa Ubungo kupitia CHADEMA ndiye mpambe wa mwenyekiti wa chama hicho taifa, Freeman Mbowe hivyo wanatafuta namna ya kumuondoa na kukihama chama.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa