Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Hawanijui Vizuri" - Sumaye

Jumatatu , 9th Jul , 2018

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye amesema watu waliodhani kwamba angeshindwa kuitikia wito wa Rais John Magufuli kwenda Ikulu wakati viongozi wakuu wastaafu wote walipoalikwa watakuwa hawamjui kwani kwenda kwake ilikuwa nafasi muhimu ya kuzungumza na kiongozi huyo kuhusu masuala ya -

Waziri Mkuu Mstaafu, Frederick Sumaye

kitaifa.

Sumaye amebainisha hayo wakati akizungumza kwenye kipindi cha Weekend BreakFast kinachorushwa siku ya Jumamosi na East Africa Radio na kusema alifurahi mupata mualiko huko kwani aliona ni fursa muhimu ya yeye kuweza kupata nafasi ya kutoa ushauri wake.

"Nilifurahi sana kupata mualiko wa Ikulu, nilijua nitaweza kupata nafasi ya kusema, niliitumia nafasi ile vizuri sana kumwambia Rais yale ninayoyafikiria wala siyo kumueleza ya kwangu binafsi bali yale ya taifa kwa ujumla. Hivyo waliofikiri tofauti kwamba sitakwenda basi hao ni watu ambao hawanijui vizuri", amesema Sumaye.

Mbali na hayo, Waziri Mkuu huyo Mstaafu amebainisha kwamba sababu kuu iliyomfanya yeye na baadhi ya viongozi wenzake kuhama Chama Cha Mapinduzi (CCM) mnamo mwaka 2015 ilikuwa ni kwenda kuongeza nguvu katika  chama cha upinzani.

"Tulitoka CCM kuja CHADEMA ili kuongeza nguvu huku ili mabadiliko yatakapotokea yasitokee upande huu mwingine ukiwa na hasira. Vipo vitu vingi ambavyo tumepandisha sana upinzani mpaka sasa", amesisitiza Sumaye.

Julai 03, 2018 Rais Magufuli aliwaalika viongozi wakuu wastaafu wote na kufanya nao mazungumzo Ikulu Jijini Dar es salaam ambapo waalikwa walikuwa ni Rais wastaafu wa awamu zilizopita, Makamu wa Rais, Mawaziri Wakuu, Maspika na Majaji Wakuu.

Sumaye alikuwa Waziri Mkuu wa awamu ya tatu katika serikali iliyokuwa ikiiongozwa na Rais Mstaafu Benjamin William Mkapa na alihama CCM mwaka 2015 wakati wa uchaguzi mkuu kwa madai ya kwamba anaunga mkono  mabadiliko yaliyokuwa yakinadiwa na upinzani.
 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava