Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Hivi ndivyo mnunua madini alivyotoa roho ya mtu

Jumapili , 27th Nov , 2022

Jeshi la Polisi mkoa wa Mbeya linamshikilia Ezekia Luhweshe (31) mchimbaji na mnunuzi wa madini, wilayani Chunya, mkoani Mbeya kwa tuhuma za mauaji ya wakala wa maegesho ya magari aitwaye William Mgaya (58) mkazi wa Mama John jijini Mbeya.

William Mgaya (58)

RPC Mbeya, ACP Benjamin Kuzaga, amesema tukio hilo limetokea Novemba 26, zilipo ofisi za TARURA katika jengo la TAFISA lililopo Kata ya Ruanda jijini humo, ambapo imeelezwa marehemu akiwa na mwenzake walimkamata Ezekiel, baada ya ku-scan namba yake ya gari T.772 DVY Toyota Hilux na kugundua kuwa gari hilo lina deni la sh.7,500.

Mtuhumiwa alitakiwa kulipa deni hilo lakini alihitaji kuona hilo deni linatokana na maegesho gani hivyo kulazimika kuongozana naye hadi zilipo ofisi za TARURA kwa ajili kuangalia kwenye mfumo ili kupata taarifa za deni hilo. 

Mtuhumiwa alionyeshwa taarifa za deni hilo na kuridhika kuahidi kulipa deni hilo lakini wakala Mgaya alimtaka kulipa deni hilo papo hapo kutokana na deni hilo kuwa la muda mrefu ndipo yalitokea majibizano kati ya marehemu na mtuhumiwa hali iliyopelekea mtuhumiwa kutoa silaha yake Pistol na kufyatua  risasi moja uelekeo alipokuwa Mgaya  na kumpiga sehemu ya kifuani upande wa kulia na kusababisha kifo chake muda mfupi baada ya kufikishwa Hospitali ya Rufaa Mbeya kwa matibabu.
 
Mtuhumiwa pamoja na Silaha Pistol aina ya Tisasi yenye namba T.0620-19J0037 ya mtuhumiwa ikiwa na risasi tisa ndani ya magazine anashikiliwa na Jeshi la Polisi.

Kamanda Kuzaga ACP ametoa rai kwa wananchi kuacha tabia ya kujichukulia sheria mkononi na badala yake watoe taarifa za malalamiko yao au kitendo chochote wanachofanyiwa kinyume cha sheria au taratibu zilizopo kwa viongozi wa mamlaka husika kwa ajili ya ufuatiliaji na hatua zaidi za kisheria.
 
Aidha Kamanda Kuzaga ametoa wito kwa wale wote wanaomiliki silaha kuzingatia masharti ya umilikishwaji wa silaha hizo pamoja na kuhakikisha silaha hizo wanazitumia kulingana na hitaji au mahitaji ya msingi waliyoombea silaha hizo na sio kutishia ama kuua watu jambo ambalo ni kinyume cha sheria za nchi na masharti ya umiliki wa silaha.

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA