Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Jinsi mvua ilivyoua watu saba Arusha

Ijumaa , 24th Feb , 2017

Jeshi la Polisi mkoani Arusha limethibitisha kutokea kwa vifo vya watu 7 kutokana na mvua kubwa iliyonyesha katika maeneo mbalimbali ya mkoa huo usiku wa jana.

Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha

Akitoa taarifa hiyo leo, Kamanda wa Polisi Mkoani Arusha ACP Charles Mkumbo amesema katika tukio la kwanza jana saa 4:00 usiku katika kijiji cha Kimbolo wilayani Arumeru, watu watano wote wakazi wa kijiji cha Kyoga walifariki dunia baada ya gari aina ya Toyota Premio lenye namba za usajili T 579 BSG kusombwa na maji.

Amewataja watu hao waliofariki katika tukio hilo kuwa ni Shengai Saiguran (30), Nembris Mungaya (20), Minis Loyi (25), Inoti George (40) na Ngaisi Moluo ambaye umri wake bado haujafahamika mara moja huku dereva wa gari hilo Yusuph Jacobo akinusurika.

Kamanda Mkumbo amesema mbali na vifo vya watu hao pia watu wengine wawili walifariki dunia katika maeneo tofauti ambapo katika kijiji cha Keriani mtu aitwaye Babu Robikeki alisombwa na maji kisha kufariki dunia wakati anavuka mto wakati akitokea matembezini.

Mtu wa katika matukio hayo ni Seuli Meseyeki (37) dereva wa bodaboda ambaye alikuwa anaendesha pikipiki aina ya T-Better yenye namba za usajili T. 726 DFD ambaye alisombwa na maji eneo la Olorieni Ngaramtoni wakati anavuka barabara.

Kamanda Mkumbo pia amesema pikipiki aina ya Boxer yenye namba za usajili MC 892 ACR iliokotwa maeneo ya Olasiti kwa Mawala halmashauri ya jiji la Arusha huku dereva wake hajulikani alipo. 

 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava