Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Lema atuma ombi kwa Rais Magufuli

Jumapili , 16th Dec , 2018

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema amemuomba Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. John Magufuli kuzungumza na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania Prof. Florens Luoga kwa kile alichodai kuwa ametoa kauli tata.

Mbunge wa Arusha Mjini (CHADEMA), Godbless Lema .

Lema kupitia ukurasa wake wa kijamii leo, Disemba 16, ameandika kuwa kauli ya Gavana ambayo hakuianisha ni kauli ipi, kuwa endapo isipoeleweka hata kama iliongelewa kwa nia njema itakuwa ni hatari kwa mstakabali wa uchumi.

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. John Pombe Magufuli akisalimiana na Gavana wa Benki Kuu ya Tanzania (BOT) Profesa Florens Luoga aliyefika Ikulu kwa ajili ya mazungumzo.

"Mh Rais tafadhali kwa heshima kabisa ongea na Gavana wa Benki kuu ,kwa maoni yangu Gavana anaongea sana.Kauli ya Gavana hata kama ina nia njema ikishindwa kueleweka mara nyingi huwa ni hatari kwa uchumi na uimara wa shilingi. Sina uhakika kama utadumu naye muda mrefu kazini", ameandika Lema.

Novemba 20, katika mkutano wake  na wanahabari, Prof. Luoga alisema kuwa taasisi hiyo imeanzisha operesheni maalum ya ukaguzi na udhibiti wa uendeshaji biashara ya fedha jijini Arusha, ikiwa ni siku moja tangu kutokea sintofahamu katika biashara ya maduka ya kubadilishia fedha jijini humo baada ya kufungwa kwa saa kadhaa.

Uchunguzi wa Benki Kuu umebaini kuongezeka biashara ya ubadilishaji na utakatishaji fedha. Kuna maduka hayajasajiliwa lakini yanafanya biashara hii kinyume cha utaratibu,” alisema Profesa Luoga.

HABARI ZAIDI

Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Afrika Mashariki, Mheshimiwa January Makamba

Ziara ya Rais Samia Korea kuanza rasmi Mei 31 2024

Bw. Nazar Nicholas (katikati) akikabiziwa tuzo ya WSIS 2024

Tanzania yashinda Tuzo WSIS 2024, nchini Uswisi

Dkt. Selemani Jafo, Waziri wa Nchi Ofisi ya Makamu wa Rais (Muungano na Mazingira).

Hati miliki ardhi za kimila 4,450 kutolewa Mei 29

DCP David Misime, Msemaji wa Jeshi la Polisi Tanzania

Mtoto atekwa na mzazi wake ili ajipatie milioni 20