Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Lugola aweka wazi waliopatikana baada ya kutekwa

Jumamosi , 13th Oct , 2018

Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Kangi Lugola, amesema Jeshi la polisi linaendelea na mchakato wa kumtafuta mfanyabiashara maarufu Mohammed Dewji "Mo Dewji" aliyetekwa siku ya Alhamis Oktoba 11,2018 jijini Dar es slaam.

Mohammed Dewji kushoto na Kangi Lugola

Akizungumza na waandishi wa habari ofisini kwake leo, Kangi amesema takribani watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi ili kusaidia kutoa ushirikiano wakati wakiendelea kuwasaka watu wote waliohusika na tukio la utekaji ikiwemo kumpata Dewji mwenyewe.

''Niwahakikishie watanzania, jeshi la polisi linaendelea kushughulikia tukio la kutekwa kwa Mohamedi Dewji, likiwasaka waliomteka na tutahakikisha wanapatikana, ambapo hadi sasa navyozungumza takribani watu 20 wanashikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano'', amesema.

Mh. Lugola pia amemtaka IGP Simon Sirro kutoa maelekezo kwa askari wake, kuwaachia ndani ya saa 24 watu wanaowashikilia kwa uchunguzi kuhusiana na kutekwa kwa Mohammed Dewji mara baada ya kuwahoji na kubaini wahusika au hawana taarifa kamili.

Aidha akisoma taarifa ya matukio ya uharifu yaliyotokea nchini tangu mwaka 2016, Kangi amesema jeshi la polisi linaendelea kuwashikilia watuhumiwa wa matukio ya kiharifu na kuwataka wananchi kuacha minong'ono kwamba serikali na vyombo vya usalama havifanyi kazi ipasavyo.

Mwaka 2016 Watu 5 kati ya 9 waliokuwa wametekwa walipatikana wakiwa hai, huku watu 27 waliotekwa  mwaka 2017, 22 wamepatikana huku watatu wakiwa hawajapatikana.

Aidha takwimu za watoto walioripotiwa kupotea kuanzia Januari hadi Oktoba mwaka huu ni 21, ambapo watoto 17 wamepatikana wakiwa hai na watoto 4 hawajapatikana hadi sasa.
 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto