Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Maagizo waliyopewa askari 8 wa kesi ya madini

Alhamisi , 18th Jul , 2019

Mkurugenzi wa mashtaka nchini Biswalo Mganga, amefuta kesi 75 zinazowakabili mahabusu na wafungwa mbalimbali katika gereza kuu la Butimba mkoani Mwanza na kuwataka wahusika kutorudia makosa.

Miongoni mwa askari 8 walioachiwa huru pamoja na mahabusu wengine.

Miongoni mwa kesi zilizofutwa ikiwemo kesi namba moja ya uhujumu uchumi ya mwaka 2019, iliyokuwa ikiwakabili askari polisi nane waliohusika na utoroshaji wa madini  kilo 319 yenye thamani ya shilingi bilioni 27.

Hatua hiyo imekuja siku moja baada ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dr. John Pombe Magufuli, kutembelea gereza kuu la Butimba na kuzungumza na wafungwa pamoja na Mahabusu.

Wakizungumza na waandishi wa habari Waziri wa katiba na sheria Balozi Agustino  Mahiga pamoja na mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP Biswalo Mganga mara baada ya kufanya ziara katika gereza hilo na kuzungumza na wafungwa na Mahabusu kwa zaidi ya saa 7, wamebaini baadhi ya waliomo katika gereza hilo wamebambikiwa kesi.

''Wapo waliobambikiziwa kesi lakini sio mahabusu wote waliopo gerezani hapo wamebambikiziwa wengine ni kweli wahusika wa kesi, niwaombe tu waendapo uraiani hali ikaendelee kuwa shwari kama ilivyokuwa wakati wakiwa gerezani'', amesema Biswalo.

Katika ziara iliyofanywa na Waziri wa katiba na sheria na Balozi Agustino  Mahiga pamoja na mkurugenzi wa Mashtaka nchini DPP Biswalo Mganga wametembelea magereza mbalimbali ya mikoa ya kanda ziwa na kufuta jumla ya kesi 325.
 

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa