Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

'Madaktari mna''Stress'', - Waziri Jafo

Jumanne , 20th Aug , 2019

Waziri wa Ofisi ya Rais TAMISEMI, Selemani Jafo amesema asilimia kubwa ya madaktari walioko nchini wana msongo wa mawazo kutokana na kazi kubwa ya kuhudumia watu waliyonayo.

Waziri Jafo ameyabainisha hayo leo Agosti 20 alipokuwa akizungumza na Waganga Wakuu wa Mikoa katika mkutano wao mkuu wa tatu uliofanyika mkoani Dodoma, ambapo amewapongeza kwa kazi yao kubwa, kwani wamekuwa wakijituma na kuwa mstari wa mbele kuokoa maisha ya watanzania.

''Niwapongeze madaktari wa Tanzania kwa kazi kubwa mnayoifanya, hili naomba nilisisitize nazungumza kwa dhati ya moyo wangu,  madaktari wetu mnafanya kazi kubwa sana ya dhati iliyopitiliza na mimi wakati wote nikiona mtu anabeza kazi ya madaktari huwa napata huzuni sana", amesema Jafo.

"Nimefika nilikuwa nawaangalia, wengi sana naona mna 'stress', mkutano umepooza,  ninachoamini kwamba wengi mnastress lakini stress hizo ni kwa kazi kubwa mnazofanya'' ameongeza Waziri Jafo.

Aidha katika pongezi zake  Waziri Jafo, ameeleza ni kwa namna gani aliwaona wakijitoa kuhudumia majeruhi wa ajali ya kulipuka kwa tenki la mafuta mkoani Morogoro.

''Mfano mzuri ni wa tukio kubwa la tenki la mafuta kuwaka moto Morogoro,nimefika pale mpaka saa tano za usiku, niliwaona madaktari hata mioyo
imeshakufa ganzi, watu waliokuwa katika hali mbaya, madaktari wakijituma kuwasindikiza Muhimbili
".

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa