Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Matendo ya polisi yamshangaza Katibu wa Mbunge

Jumatatu , 18th Sep , 2017

Katibu wa Mbunge wa Tarime Vijijni John Heche, Mrimi Zabloni amesema analishangaa Jeshi la Polisi nchini kwa kukamata watu wanaokusanyika kumuombea Tundu Lissu na kuruhusu matamasha yanayofanyika usiku kucha huku viongozi wa mikoa wakishiriki.

Mrimi amefunguka hayo wakati akizungumza kwa njia yasimu na Mwandishi wa EATV na kusema kwamba anasikitisha na vitendo vinavyofanywa na jeshi la polisi kukataza mikusanyiko ya wanachadema badala ya kuipa ulinzi.

"Kuna vitu hawa askari polisi wetu wanafanya vya kushangaza, kuna matamasha mengi yanafanyika usiku na viongozi wa mikoa wanashiriki lakini maombi ya Lissu yanayofanywa mchana kweupe wanayapinga, sijui tunaelekea wapi. Kati ya matamasha ya usiku na maombi yapi yanahatarisha amani? Wenzetu Kenya jana wamefika hadi hospitalini na kufanya ibada kwa ajili ya kumuombea Lissu kwa nini hatujifunzi kutoka huko? alisisitiza kwa njia ya kuhoji.

Aidha Mrimi amewataka watu kutohusisha tukio la Tundu Lissu kama mtaji wa siasa kwa Baraza la Vijana Chadema (BAVICHA) na kwamba harakati zinazofanywa na vijana hao ni kuhakikisha wanatoa hisia zao juu ya matatizo aliyoyapata mwanasheria wao.

Amesema kuwa wanachokifanya Bavicha siyo siasa bali wanatumia uhuru wa Katiba na kwa mujibu wa sheria ya vyama vingi nchini kwani wanaruhusiwa kuzungumza na hata kuandamana ili kutoa hisia zao kwa mambo yanayoendelea nchini.

"Wanaosema Bavicha wanamtumia Lissu kama mtaji wa kisiasa ni mtazamo wao tu, kwani naamini wanafanya kazi kwa mujibu wa heria na katiba hayo mengine ni hila tu. Naamini wamekumbwa na matatizo mengi viongozi kupotea, misukosuko ya viongozi wa chama lakini pia hata mauaji yaliyowahi kutokea kwa viongozi na shambulio la Lissu kwa hiyo ni haki yao kama vijana kupaza sauti kukemea" Mrimi aliongeza
 

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava