Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam, Paul Makonda
Hayo ameyabainisha leo Novemba, 5, 2019, alipotembelea watoto wanaopatiwa matibabu ya moyo katika Taasisi ya Moyo, Jakaya Kikwete Cardiac Institute (JKCI) na kuwaomba watanzania kuendelea kujitokeza kwa wingi ili kuokoa uhai wa watoto wenye uhitaji.
"Mimi ningekuwa na uwezo wa kutunga sheria, binafsi ningesema mtu akikukwangua bampa achana naye tu wewe shuka kwenye gari angalia bampa yako, mwambie pole kwasababu wala hukukusudia.", amesema Makonda.
"Kuna watu mkiguswa tu bampa ya Vits au Ist mnabaki mpaka msongamano wa magari unakuwa mkubwa, ukiguswa kidogo kama gari yako haijaharibika msamehe tu mwenzio.", ameongeza Makonda.
Aidha Makonda amesema kuwa anataka kuufanya mwezi Disemba kuwa ni wa shukrani kwa kuwainua watoto wenye matatizo ya moyo wanaopitia maumivu makali huku wakiwa hawana tumaini lolote la kupona na kuwapeleka katika viwango vingine.