Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Nape apinga mfumo wa serikali kudhibiti 'kangomba'

Jumanne , 11th Dec , 2018

Mbunge wa Jimbo la Mtama, Nape Nnauye ameibuka na kuwatetea wakulima baada ya serikali kutangaza hivi karibuni kuanza kutowalipa pesa wakulima wanaomiliki korosho walizozipata kwa kuzinunua kutoka kwa wenzao kwa mfumo wa 'kangomba' pasipo kuwa na mashamba.

Nape Nnauye

Nape amesema kuwa mfumo huo unaoendelea sasa unawapa mateso wakulima na kupendekeza kuwa ili kumaliza tatizo hilo, ni vyema serikali kuviwezesha vyama vya ushirika kupitia Benki ya Maendeleo ya Wakulima (TADB) kulipa sehemu ya malipo kwa wakulima hao mara tu korosho inapofika ghalani.

Kupitia ukurasa wake wa Twitter, Nape Nnauye ameandika, "dawa ya kangomba ni kubadili mfumo wa malipo ya korosho kwa wakulima, kwa kuviwezesha Vyama vya Ushirika kupitia TADB kulipa sehemu ya malipo mara tu korosho inapofika ghalani".

"Hiki kinachoendelea sasa hakiwezi kumaliza kangomba, ni mateso tu kwa wakulima!," ameongeza Nape.

Rais Magufuli wakati akitangaza uamuzi wa serikali kununua korosho za wakulima, Novemba 13 Jijini Dar es salaam alisema kuwa serikali itanunua korosho zote za wakulima kwa bei ya sh 3,300 kwa kilo baada ya wanunuzi binafsi kushindwa kutimiza matakwa ya serikali.

Hivi karibuni Mkuu wa Wilaya ya Nachingwea, Rukia Muwango alisema kuwa wakulima wote waliouza zao hilo bila kuwa na mashamba, wajiandae kisaikolojia kwani hawatolipwa mpaka watakapoonesha mashamba waliyovuna korosho hizo.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava