Katika taarifa hiyo, NBS imesema kuwa wanajiandaa kufanya utafiti wa watu wenye uwezo wa kufanya kazi utakaofanyika mwaka 2019/20 na ilifanya makisio ya mwenendo wa hali ya soko la ajira kwa 2018.
"Matokeo ya takwimu hizo yanaonesha kuwa idadi ya watu walio na ajira imeongezeka kutoka milioni 20.0 mwaka 2014 hadi milioni 22.0 mwaka 2018", imesema sehemu ya taarifa hiyo.
Takwimu hizi hutumika pia kama kigezo cha kufanya maoteo ya hali ya ajira katika vipindi ambavyo hakuna tafiti zilizofanyika ili kutoa hali ya soko la ajira katika vipindi vifupi vifupi.
"2017/18 kulikuwa na jumla ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini ikilinganishwa na ajira 453,466 kwa mwaka 2016/17, hili ni ongezeko la ajira 98,597 sawa na asilimia 21.7 kati ya mwaka 2016/17 na mwaka 2017/18."
Aidha NBS imefafanua kuwa kati ya ajira 552,063 zilizozalishwa nchini mwaka 2017/18, ajira 415,009 sawa na asilimia 75.0 zilikuwa ni ajira kutoka Serikalini, ajira hizi zinajumuisha ajira 18,000 kutoka Serikali Kuu na ajira 397,009 kutoka katika miradi ya maendeleo kupitia Mpango wa Pili wa Maendeleo wa Taifa wa m