Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

NEC yaijibu taarifa ya ubalozi wa Marekani

Alhamisi , 16th Aug , 2018

Tume ya Taifa ya Uchaguzi (NEC) imetoa ufafanuzi kuhusiana na madai ya ubalozi wa Marekani nchini iliyoyatoa katika taarifa yake hapo jana kuhusu uchaguzi mdogo wa Agosti 12 kwenye jimbo la Buyungu na kata 36 nchini.

Katika taarifa iliyotolewa na  NEC, kupitia  Ofisa Habari Mwandamizi NEC Christina Njovu tume imeutaka ubalozi huo uthibitishe inachokieleza juu ya uchaguzi mdogo wa Jimbo la Buyungu na kwenye kata 36 ikisema uchaguzi mdogo huwa hauna waangalizi wa kimataifa na kuhoji ubalozi wa Marekani umetoa wapi taarifa hizo na hayo ulioyaona ni kwa kutumia utaratibu upi na sheria ipi ?.

Katika Jimbo la Buyungu mgombea wa ubunge wa Chadema Elia Kanjaro aliongea na vyombo vya habari na kwenye mitandao ya kijamii akaeleza hisia zake na kusema bayana kuwa amekubaliana na matokeo na ameshukuru kwa kuwa uchaguzi huo umemjenga,”  inasema taarifa hiyo ya NEC.

Taarifa hiyo imeongeza kuwa kilichotokea Arusha ni vurugu mitaani mbali na maeneo ya vituo vya kupigia kura, kwa kuwa vurugu hizo zilipelekea jinai kufanyika vyombo husika vinashughulikia. "Hakuna chama chochote kilichojitokeza kusema na kuthibitisha kuwa uchaguzi haukuwa huru na haki," imesema taarifa hiyo.

Hatua hiyo imekuja kufuatia taarifa iliyotolewa na Ubalozi wa Marekani nchini kuhusu uchaguzi wa marudio katika Kata 77 na jimbo la Buyungu uliofanyika mnamo Agosti 12, 2018 ambapo kwa mujibu wa taarifa kutoka katika ofisi za ubalozi huo imeeleza kuwa uchaguzi huo uligubikwa na matukio ya fujo na ukiukwaji wa kanuni za uchaguzi.

HABARI ZAIDI

Mwenyekiti Jukwaa la Wahariri Tanzania, Deodatus Balile

Balile achaguliwa kuwa Mwenyekiti EAES

Mhe. George Simbachawene, Waziri wa Nchi, Ofisi ya Rais, Menejimenti ya Utumishi wa Umma na Utawala Bora

Waliohitimu mafunzo ya uongozi wafundwa uadilifu

Mkuu wa mkoa wa Katavi Mwanamvua Mrindoko,

Wadau wa afya simamieni ukusanyaji mapato

Picha za Kuonesha Muelekeo wa Kimbunga IALY

Kimbunga IALY charipotiwa bahari ya Hindi

Mabaki ya Nyumba yenye vyumba 12 iliyoteketea na Moto

Moto wateketeza nyumba yenye vyumba 12

Baadhi ya Majirani wa Kijana Amani Abed ambaye Amejinyonga baada ya kutoka Hospitali.

Kijana ajinyonga baada ya kutoka hospitali

Antony Blinken, Waziri wa Mambo ya Nje wa Marekani

Marekani yatangaza kulifadhili jeshi la Ukraine