Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

"Nimerudi na unyenyekevu"- Zitto

Jumatatu , 18th Sep , 2017

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe amefunguka na kudai amerudi nchini akiwa na unyenyekevu mkubwa zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri alionyeshwa na Mbunge Tundu Lissu pindi alipokwenda kumjulia hali katika hospitali ya Nairobi nchini Kenya.

Mbunge wa Kigoma Mjini Zitto Kabwe.

Zitto ameeleza hayo kupitia ukurasa wake wa facebook asubuhi ya leo na kusema japo Lissu ameumizwa sana lakini hakuacha kumuonyesha ucheshi licha ya kuwa na maumivu makali aliyokuwa nayo katika mwili wake.

"Siku mbili hizi nilizoenda kumuona Lissu zimeniacha nikiwa mawazo sana, nimerudi nchini nikiwa kwenye unyenyekevu zaidi kwa sababu ya nguvu na ujasiri ambao ndugu yangu amenionesha licha ya kuwa kwenye maumivu makali. Siyo mara nyingi hapa nchini kusikia tukiongelea ujasiri lakini namfikiria lissu na vile nilivyojisikia nikiwa pamoja naye Nairobi, najua hivyo ndivyo alivyo", ameandika Zitto.

Pamoja na hayo, Zitto ameendelea kwa kusema "waliomshambulia wamemuumiza kweli na bado wakati tuliokuwa naye amenionesha shukrani, ari na pia ucheshi. Huo ni ujasiri, alichopitia na anachoendelea kupitia Lissu siyo kitu rahisi kwa mtu yeyote kutafakari. Kufikiria hali ile kungeniacha niumie moyo kama asingesema maneno haya kwangu kuwa  'tumeshinda. Tumeshashinda", amesisitiza Zitto.

Mbunge Tundu Lissu alishambuliwa kwa risasi na watu wasiojulikana Septemba 7, 2017 akiwa Makao Makuu ya nchi mjini Dodoma na baadaye kusafirishwa kwenda jijini Nairobi Kenya kwa ajili ya kupatiwa matibabu kufuatia majeraha aliyopata, ambapo mpaka sasa yuko huko kwa matibabu.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa