Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Prince Philip wa Uingereza afariki dunia

Ijumaa , 9th Apr , 2021

Mume wa Malkia Elizabeth wa Uingereza, Prince Philip, (Duke of Edinburgh) amefariki dunia.

Prince Philip

Taarifa iliyotolewa na familia hiyo ya kifalme inasema kuwa Prince Philip amefariki asubuhi ya leo akiwa katika Jumba la kifalme (Windsor Castle) na umri wa miaka 99.

Waziri Mkuu wa Uingereza Boris Johnson anasema ni "kwa huzuni kubwa" kupokea habari za kifo cha Mwanamfalme Philip kutoka Kasri la Buckingham.

Akitoa salamu zake za rambirambi alisema Mwanamfalme Philip alipata mapenzi ya vizazi nchini Uingereza, katika Jumuiya ya Madola na ulimwenguni kote

"Alikuwa mshirika wa kifalme aliyehudumu kwa muda mrefu katika historia, mmoja wa watu wa mwisho nchi hii kuwahi kutumika katika Vita vya pili vya na alitajwa katika barua za ushujaa."

Malkia Elizabeth wa Uingereza akiwa na mume wake Prince Philip enzi za uhai wake

Katika rambirambi zake, Boris Johnson alisema, "alisaidia kuongoza familia ya kifalme na ufalme ili iweze kuwa taasisi muhimu bila shaka kwa usawa na furaha ya maisha yetu ya kitaifa."

Boris Johnson anamaliza rambi rambi zake kwa kusema kwamba Familia ya Kifalme wamepoteza "sio tu mtu anayependwa sana na anayeheshimiwa sana na umma, lakini mume aliyejitolea, baba mwenye fahari na mwenye upendo, babu, na katika miaka ya hivi karibuni, babu-mkubwa".

Waziri mkuu anamnukuu Malkia wakati mmoja akisema nchi hiyo inadaiwa na mumewe deni kubwa kuliko "tunavyopaswa kujua", na kuongeza kuwa alikuwa na hakika kuwa makadirio hayo yalikuwa sahihi.

'Tunaomboleza leo na Malkia, tunampa pole zetu, na familia yake yote na tunashukuru, kama taifa, na ufalme, kwa maisha ya kipekee na kazi ya Mwamfalme Philip, Mtawala wa Edinburgh," alisema.

HABARI ZAIDI

Mkuu wa Mkoa wa Arusha, Paul Makonda (Mwenye shati ya Bluu) akipata maelekezo wakati wa maonesho ya OSHA 2024 kwenye Viwanja vya General Tyres jijini Arusha.

RC ataka GGML iboreshe maisha ya wananchi Geita

Vijana Waliojiajiri Sekta ya Kilimo, Nigeria

Mishahara yaongezeka nchini Nigeria

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa