Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Rais Magufuli ataja rasmi muda atakaohamia Dodoma

Jumapili , 14th Oct , 2018

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt John Pombe Magufuli amesema kuwa mwezi wa kumi na mbili mwaka huu anatarajia kuhamia rasmi makao makuu ya nchi Dodoma kama ilivyokuwa matamanio ya Hayati Mwalimu Julius Nyerere.

Rais, Dkt John Magufuli

Rais Magufuli ametoa kauli hiyo jijini Dar es salaam wakati alipokwenda kumtembelea Mjane wa Baba wa Taifa, Mama Maria Nyerere ambapo kabla ya kufika kwake alitumia fursa hiyo kushiriki nae ibada kanisa la Mtakatifu Petro Oysterbay.

Rais Magufuli amesema “azimio la Arusha ukilisoma unajua kila kitu kuhusu nchi yetu, baba wa taifa mwaka 1973 alisema tuhamie Dodoma ndio makao makuu ya nchi, Dodoma tunahamia na mimi ndio nakaribia kumalizia, mwezi wa 12 nihamie huko.”

“Niwaombe watanzania wenzetu tuendelee kuitunza amani yetu, maana hatuna baba mwingine wakutusimamia zaidi ya baba wa mbinguni, lakini kifo cha baba wa taifa kitufunze watanzania tuwe na mshikamano, na kila mmoja tuendelee kumuombea huko aliko aendelee  kupumzika kwa amani, ameongeza Rais Magufuli.

Kitaifa kumbukumbu ya Mwalimu Nyerere inafanyika Mkoani Tanga, ambapo mamia ya wananchi wamejitokeza na kushuhudia sherehe hizo ambazo Mgeni rasmi ni Rais wa Zanzibar, Dkt Ally Mohamed Shein.

Oktoba 14 ndio tarehe ambayo Watanzania tunaadhimisha kifo cha Muasisi wa Taifa Mwalimu Julius Nyerere ambacho kilitokea mwaka 1999 baada ya kuugua kwa muda nchini Uingereza.

HABARI ZAIDI

Picha za Satelaiti Zikionyesha Mwenendo wa Kimbunga Hidaya

Kimbunga Hidaya chaendelea kutawala eneo la Pwani

Madaktari Bingwa wa Mama Samia Wakiendelea na Upasuaji

Uvimbe wa kilo 5 waondolewa tumboni kwa mwanamke

Rocket Mwashinga, Chifu Mkuu wa Kabila la Wasafwa

Chifu Mwashinga akemea washirikina kutesa watu

Waziri Mkuu Mhe. Kassim Majaliwa akizungumza na Wanahabari na Wadau wengine kwenye Maadhimisho ya Siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari Duniani yaliyofanyika kwenye Ukumbi wa Mikutano wa Jakaya Kikwete, jijini Dodoma leo Mei 03, 2024.

Watendaji serikalini ondoeni ukiritimba - Majaliwa

Kamanda wa Polisi mkoa wa Morogoro SACP Alex Mkama, akionesha vitu vilivyokuwa vimeibiwa

Fundi ujenzi mbaroni mauaji ya dada wa kazi

Wahitimu wa Mafunzo ya Jeshi la Kujenga Taifa JKT

Wahitimu JKT watakiwa kulinda miradi ya serikali

Daktari wa GGML aliyebobea katika magonjwa yatokanayo na kazi, Cretus Karwan akimpatia vipimo mmoja wa wananchi waliotembelea banda la GGML na kupatiwa huduma za awali za upimaji wa afya katika maonesho ya OSHA yanayoendelea jijini Arusha.

Wananchi 200 wapimwa afya maonesho ya OSHA

Rais wa Shirikisho la Vyama vya Wafanyakazi Tanzania (TUCTA), Tumaini Nyamhoka akipokea zawadi kutoka kwa Ofisa Mwandamizi wa masuala ya jamii na maendeleo ya kiuchumi kutoka GGML, Ruth Mharagi alipotembelea banda la GGML katika maonesho ya afya na usalama mahali pa kazi jijini Arusha.

TUCTA, OSHA wataka kampuni za madini kuiga ubunifu