Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Sababu za Meya wa Jiji la Dar kushikiliwa Polisi

Jumapili , 2nd Dec , 2018

Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita jana Jumamosi Desemba Mosi, 2018 alikamatwa na Jeshi la Polisi Kanda Maalum ya Dar es Salaam, ambpo kwa mujibu wa ripoti anaendelea kushikiliwa hadi sasa.

Meya wa Jiji la Dar es salaam, Isaya Mwita.

Kamanda wa Polisi Kanda Maalum ya Dar es salaam, Lazaro Mambosasa amesema kuwa sababu ya Mwita kukamatwa ni kitendo chake cha kuongoza maandamano bila kuwa na kibali.

Tulipomkamata akaeleza alikuwa anakwenda kuzindua kisima cha maji ambacho hakukijenga yeye kilijengwa na serikali kupitia kwa mheshimiwa DC aliyehamia Ruangwa. Sasa yeye alikuwa anataka kupora ili kutafuta sifa kwamba alijenga yeye wakati mradi ni wa Serikali, aliokuwa amewaalika walikimbia wote,” amesema Mambosasa.

Aidha Kamanda Mambosasa amesema kuwa Jeshi la Polisi linaendelea kumshikilia Meya huyo hadi pale upelelezi utakapokamilika, baadaye atafikishwa mahakamani.

Kwa upande wao CHADEMA kupitia Mkurugenzi wa Itifaki, Mawasiliano na Mambo ya Nje wa chama hicho, John Mrema amesema Meya huyo jana alikuwa na mkutano na baadhi ya wananchi wa kata ya Vijibweni kabla ya kuzindua matawi mapya, ambapo walipokuwa wakielekea katika uzinduzi wa matawi hayo polisi waliwavamia na kuwakamata.

Manadamano hayo yalifanyika katika kata ya Vijibweni, wilayani Kigamboni kuelekea daraja la Mwalimu Nyerere, ambapo Meya Mwita pia ni diwani wa kata ya Vijibweni Kigamboni kwa tiketi ya CHADEMA.

HABARI ZAIDI

Coaster iliyoparamia nyumba Bukoba

Tisa wanusurika kifo Kagera

Picha ya Fat Joe na Chris Brown

"Chris Brown anafaa kuwa 2Pac wa kisasa" - Fat Joe

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji