Error message

  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 664 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 670 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 667 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 675 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Notice: Trying to access array offset on value of type null in amp_node_view() (line 679 of /home/eatv/public_html/sites/all/modules/amp/amp.module).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).
  • Warning: "continue" targeting switch is equivalent to "break". Did you mean to use "continue 2"? in include_once() (line 3493 of /home/eatv/public_html/includes/bootstrap.inc).

Serikali kuunganisha wilaya za Lindi kwa lami

Jumatatu , 11th Apr , 2016

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa, amesema serikali inatarajia kujenga kwa kiwango cha lami barabara ya kutoka Nanganga, Ruangwa hadi Nachingwea.

Waziri Mkuu wa Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania, Mhe.Kassim Majaliwa,

Hatua hiyo itawezesha kutatuliwa kwa kero ya changamoto ya miundombinu ya barabara inayowakabili wananchi wa wilaya za Ruangwa na Nachingwea kwa muda mrefu.

Waziri Mkuu, Majaliwa amesema barabara hiyo ambayo kwa sasa haipo katika hali nzuri itajengwa kwa kiwango cha lami, ambapo serikali inatarajia kuanza kuifanyia upembuzi yakinifu katika mwaka wa fedha wa 2016/2017.

Hayo yamesemwa jana jioni na Waziri Mkuu, Kassim Majaliwa alipozungumza kwa nyakati tofauti na wananchi wa vijiji vya Likunja, Nkowe na Namahema katika mikutano ya hadhara aliyoifanya wilayani Ruangwa wakati akiwa kwenye ziara yake ya kikazi.

Amesema serikali imejipanga katika kuboresha miundombinu ya barabara kwenye maeneo mbalimbali nchini na kwamba mara baada ya kumalizika kwa upembuzi yakinifu ujenzi wa barabara hiyo utaanza, hivyo amewataka wananchi kuwa na subira.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu, Majaliwa amewataka wananchi wa vijiji hivyo kushirikiana katika shughuli za maendeleo na kuweka kando itikadi zao za kisiasa kwa sababu uchaguzi ulishamalizika tangu Oktoba 25 mwaka jana.

“Mimi nitaendelea kuwaheshimu, kuwasikiliza na kuwahudumia, nawaomba tushirikiane na tuweke kando masuala ya itikadi za vyama, sasa ni wakati wa kazi, hivyo ni bora tukashirikiana kufanya kazi kwa maendeleo ya Ruangwa jambo ambalo linawezekana.

Hata kama wewe ambaye najua ulinichukia mimi nimekusamehe kutoka moyoni, wewe ni wangu hata kama hukunichagua nitakuhudumia na kukutumikia kwa sababu mimi ndiye mbunge wako hivyo naomba tushirikiane,” amesema.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa Halmashauri ya wilaya ya Ruangwa, Rashid Nakumbya aliomba wakazi wa wilaya hiyo kushirikiana kwa pamoja kwa ajili ya kuboresha maendeleo ya wilaya yao na hatimaye iweze kupiga hatua.

HABARI ZAIDI

Katibu wa Chadema Kanda ya Kaskazini, Amani Golugwa

Maandamano yetu sio kelele za wahuni - Golugwa

Nyumba ambayo mwili wa mwanaume ulikaa hadi kuharibika

Mke aishi na maiti ya mumewe akiamini atafufuka

Ofisa wa idara ya manunuzi na mikataba akimpatia maelezo mmoja wa wananchi wawaliojitokeza kutembelea banda la GGML katika maonesho ya OSHA na kujifunza namna kuzingatia usalama katika shughuli zao za kila siku.

GGML yaja na teknolojia za kisasa za uokoaji

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Samia Suluhu Hassan

Rais Samia asema CDF mwanamke atapatikana 2030

Mratibu wa idara ya dharura (ERT) kutoka GGML, Mohamed Mwaimu akimuonesha mama lishe namna ya kuzima moto wakati inatopokea mtungi wa gesi unapopata hitilafu na kulipuka. Mafunzo hayo yametolewana GGML kwa kushirikiana na OSHA kwa akina mama lishe 50 wa mkoani Arusha.

Mama lishe wafundishwa kulikabili janga la moto

Picha ya AY kulia na Mr II Sugu kushoto

AY Starring wa muziki wa BongoFlava